Wednesday, 31 May 2017

RAMADHAN 1438


KARIBU MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI


Al-madrasat Majalis Sania tunawatakia waislamu wote Duniani Kuifunga Ramadhani kwa Imani  hakika huu ni Mwezi ulioshushwa Qur-an,

NINI FUNGA: Swaumu ni kujiuilia kufanya jambo lolote la kawaida mtu alilolizowea kulifanya na katika sheria ya kiislamu kufunga ni kujizuia kula kunywa,kujizuia kuiniza kitu katika matundu mawili na kujizuia kumuasi Allah kuanzia Alfajir ya kweli mpaka kuingia Magharibi.

LENGO LA FUNGA: Allah taala amesema "Enyi Mlioamini mmelazimishwa kufunga{swaumu}kama walivyolazimishwa waliopita kabla yenu ili mpate kumcha Mwenyezimungu"{2:183}.
lengo la Swaumu katika Uislamu ni kumuwezesha mja wake awe Mcha Mungu kwa kufuata maamrisho yote ya Allah na kuacha makatazo yake yote.
Ili swaumu ya mfungaji iwe na maana na iweze kufikia lengo,mfungaji hana budi kujizuilia {kukifungisha kila kiungo chake cha mwili,macho,masikio,ulimi,mikono,miguu pamoja na fikra na hisia zake na matendo alioyakataza Allah taala.}..
UMUHIMU WA FUNGA YA RAMADHANI KATIKA UISLAMU:
  • Funga ya Ramadhani ni miongoni mwa nguzo ya Nne ya Uislamu na ni Faradhi kwa waislamu kama alivyosema Allah taala kwenye Quran Suratul Bakra aya ya 183
Mtu atakapoivunja makusudi hatobakia kuwa muislamu japo kua atajiita muislamu na watu wakamtambua kua muislamu na kumuita hivyo
  • Funga ni Ibada Maalumu iliomuhimu sana katika kumuandaa mja kuwa mcha mungu.
  • Funga ni ngao ya kumzuia muumini na maovu yanayosababishwa na matashi  ya kimwili na itakua ni sababu ya muumini kuingia Peponi na kuachwa huru na Moto.
NGUZO ZA FUNGA:
Nguzo za funga ni mbili  
  1. Nia
  2. kujizuia na kila chenye kufunguza tangu Alfajiri mpaka Magharibi.
YANAYOBATILISHA FUNGA
Ukifanya moja wapo katika yafuatayo,basi swaumu itabadilika.
  1. kula,kunywa na kuvuta sigara
  2. kujitapisha kwa makusudi
  3. kupata na hedhi na nifasi
  4. kujitoa manii kwa makusudi
  5. kunuia kula na hali umefunga
SUNNA ZILIZOAMBATANA NA FUNGA YA RAMADHANI:
  1. Kula na kuchelewa daku
  2. kufutari mapema
  3. Kuzidisha ukarimu
  4. Kuzidisha kusoma Quran
  5. Kusimamisha Swala ya usiku,Tarawehe
  6. Kuutafuta Usiku wa Lailatul-Qadeer
  7. kukaa Itikafu
TUNAWATAKIA RAMADHANI NJEMA
SHUKRANI
Bin Malik Khatib Zubeir
Mwalimu Mkuu
Madrasat Majalis Sania
 https://www.facebook.com/profile.php?id=100004405291677
0715721401

Monday, 20 February 2017

WALIMU NA WANAFUNZI MADRASAT MAJALIS SANIA 2017

Maalim Anasi khatib Zubeir Mwalimu Mkuu wa Madrasat Majalis Sania akinong'ona na Mc

Sheikh Thabit{kushoto} akiwa na Mwalimu Mkuu wa Madrasat Majalis Sania na pembeni yake kulia Ni Maalim Fadhil
Sheikh Fadhil na Sheikh Thabit

Thursday, 2 February 2017

Wednesday, 1 February 2017

Assalam Alaykum Warahmatullah tunategemea tarehe 18/02/2017 ndio siku ya Maulidi yetu ya kumswalia mtume muhammad (S.w.a) ambapo tunatarajia tutakua na wageni kutoka Dar-es-salam Madrasat Taalim iliopo Mwananyamala kisiwani mtaa wa sindano tumuombe Allah atufikishe Uhai na Uzima Inshallah Ratiba ya Shuhuli yetu itafuatia hapa wiki Ijayo

Chuo Cha Marehemu Bi Mkubwa Stadi

Assallam alleykum warahmatullah wabarakatuh

Je, haujafika wakati wa kuamka na kuyazingatia yale ya kutusaidia Siku ya Mwisho?
Kwani anatuuliza Allaah {{سبحانه وتعالى}}:

أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿١٦﴾

Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah na yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawatawilikia muda, kisha zikawa ngumu nyoyo zao? Na wengi miongoni mwao ni mafasiki.

{} Al-Hadiyd: 16 {}.

Tunasema Tumeamini na Masha Allaah machoni kwa watu tunaonekana waumini kweli lakini Allaah anahukumu nyoyo. Hivyo haijawa bado funzo kwetu kama Qiyaamah kipo chini ya pua zetu kinasubiri amri tu kije kwetu. Dalili ngapi tushaziona? Dalili ngapi tushazishuhudia? Twasubiri hadi milango ya tawbah ifungwe ndio turudi kwa Mola wetu? SubhaanaAllaah!

Tumegeuka  kumuasi Ar-Rahmaani, hadi kuwa sawa na wanyama wasiofahamu kitu?
Anasema Allaah {{سبحانه وتعالى}}:

وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴿١٧٩﴾

Kwa yakini Tumeumba Jahannam kwa ajili ya wengi katika majini na wanaadamu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.

{} Al-A’raaf: 179 {}.

Hivyo kila jambo la dhambi tunalolifanya ambalo wanyama hawalifanyi au wanalifanya basi tunakuwa kama wao wanyama na kuwa zaidi yao na lengo kuumbwa moto wa Jahannam Anasema Allaah {{سبحانه وتعالى}}:

وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ

Kwa yakini Tumeumba Jahannam kwa ajili ya wengi katika majini na wanaadamu.

Kwasababu gani ikawa umeumbwa kwa Binadamu na Majini anaendelea {{سبحانه وتعالى}}:

ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴿١٧٩﴾

Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.

Ee!! Nina nini mimi:

رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنْ الْمُسْلِمِينَ 

Mola wangu! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee kizazi changu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu. Aamiyn.