Wednesday, 31 May 2017

RAMADHAN 1438


KARIBU MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI


Al-madrasat Majalis Sania tunawatakia waislamu wote Duniani Kuifunga Ramadhani kwa Imani  hakika huu ni Mwezi ulioshushwa Qur-an,

NINI FUNGA: Swaumu ni kujiuilia kufanya jambo lolote la kawaida mtu alilolizowea kulifanya na katika sheria ya kiislamu kufunga ni kujizuia kula kunywa,kujizuia kuiniza kitu katika matundu mawili na kujizuia kumuasi Allah kuanzia Alfajir ya kweli mpaka kuingia Magharibi.

LENGO LA FUNGA: Allah taala amesema "Enyi Mlioamini mmelazimishwa kufunga{swaumu}kama walivyolazimishwa waliopita kabla yenu ili mpate kumcha Mwenyezimungu"{2:183}.
lengo la Swaumu katika Uislamu ni kumuwezesha mja wake awe Mcha Mungu kwa kufuata maamrisho yote ya Allah na kuacha makatazo yake yote.
Ili swaumu ya mfungaji iwe na maana na iweze kufikia lengo,mfungaji hana budi kujizuilia {kukifungisha kila kiungo chake cha mwili,macho,masikio,ulimi,mikono,miguu pamoja na fikra na hisia zake na matendo alioyakataza Allah taala.}..
UMUHIMU WA FUNGA YA RAMADHANI KATIKA UISLAMU:
  • Funga ya Ramadhani ni miongoni mwa nguzo ya Nne ya Uislamu na ni Faradhi kwa waislamu kama alivyosema Allah taala kwenye Quran Suratul Bakra aya ya 183
Mtu atakapoivunja makusudi hatobakia kuwa muislamu japo kua atajiita muislamu na watu wakamtambua kua muislamu na kumuita hivyo
  • Funga ni Ibada Maalumu iliomuhimu sana katika kumuandaa mja kuwa mcha mungu.
  • Funga ni ngao ya kumzuia muumini na maovu yanayosababishwa na matashi  ya kimwili na itakua ni sababu ya muumini kuingia Peponi na kuachwa huru na Moto.
NGUZO ZA FUNGA:
Nguzo za funga ni mbili  
  1. Nia
  2. kujizuia na kila chenye kufunguza tangu Alfajiri mpaka Magharibi.
YANAYOBATILISHA FUNGA
Ukifanya moja wapo katika yafuatayo,basi swaumu itabadilika.
  1. kula,kunywa na kuvuta sigara
  2. kujitapisha kwa makusudi
  3. kupata na hedhi na nifasi
  4. kujitoa manii kwa makusudi
  5. kunuia kula na hali umefunga
SUNNA ZILIZOAMBATANA NA FUNGA YA RAMADHANI:
  1. Kula na kuchelewa daku
  2. kufutari mapema
  3. Kuzidisha ukarimu
  4. Kuzidisha kusoma Quran
  5. Kusimamisha Swala ya usiku,Tarawehe
  6. Kuutafuta Usiku wa Lailatul-Qadeer
  7. kukaa Itikafu
TUNAWATAKIA RAMADHANI NJEMA
SHUKRANI
Bin Malik Khatib Zubeir
Mwalimu Mkuu
Madrasat Majalis Sania
 https://www.facebook.com/profile.php?id=100004405291677
0715721401

No comments:

Post a Comment