MALENGO

MALENGO YA MADRASAT MAJALIS SANIA
(BI MKUBWA STADI)
 Malengo ya madrasa ni :-
  1. kuiendeleza madrasa na kukuza masomo
  2. kuhakikisha mwanafunzi anapata maadili na kukulia katika malezi ya dini ya kiiislam 
  3. Kutafuta mbinu mbalimbali za kuwasaidia wanafunzi katika kujitayarisha na maisha
  4. kutafuta wafadhili wa kuweza kutusaidia katika harakati za kuikuza madrasa yetu
  5. kuwasaidia watoto mayatima na wasiojiweza katika zone ya kikwajuni na maeneo ya karibu
  6. kusaidia baadhi ya madrasa ambazo hazina uwezo kwa kuwatafutia wafadhili
  7. kuimarisha umoja na mshikamano baina ya vyuo na walimu wa madrasa.
  8. kupata wanafunzi wengi watakaojiunga na madrasa.
  9. kuhifadhi qur-an
  10. kushiriki katika mashindano ya QUR-AN .
  11. kutafuta walimu wa uhakika watakaojitolea katika kutoa Elimu n.k.
  12. kuandaa sare maalum kwa ajili ya kivazi cha wanafunzi wakati wa madrasa.
  13. kuandaa sherehe za maghafal  kila mwaka mara moja pmoja na futari kila ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhan.
  14. kuandaa madawati maalum(madogo) na mirfaq kwaajili ya kuwekea vitabu wakati wa masomo.
  15. Kuendeleza ujenzi wa madrasa yetu.
Matatizo yetu:-
  1. kukosa mashirikiano ya kutosha kwa baadhi ya wazazi hasa katika suala zima la maadili na malezi ya watoto pamoja na ujaji wa madrasa.
  2. kushuka kwa kiwango cha kuhifadhi MASOMO kutokana na kwanza mzazi kutomuhimiza mtoto wake na pindipo atarudi madrasa kile ambacho amepewa hakipo,istoshe pia mwalim anakua na harakati za kimaisha za kutafuta rizki na hua anakosa muda mzuri wa utulivu ili atoe elimu kwa watoto,na yote kwa sababu mwalimu wa chuoni hana kipato maalum kitakacho mkidhia haja zake.
  3. Tatizo la fedha katika kuendesha harakati za madrasa
  4. kukosa zana za kufundishia kama vile vitabu(juzuu, mas-haf,),mashine za kutayp,Photocopi mashine,printer na scana , compyuta n.k.
  5. kukosekana kwa muamko wa vijana kuwa hawataki kusoma na kuacha madrasa akiwa kijana wa miaka 15 na kuendlea mbele.
  6. kukosa walimu wa uhakika wa kutosha nk.
Mafanikio yetu:-
  1. Tumeweza kuanza ujenzi wetu kwa kuomba misaada maeneo na watu tofauti kupitia katika mtandao wa kijamii Facebook nsa umekamilika kiasi cha kua sihaba kunasomeka ingawa haijakamilika.
  2. Tumeweza kuwasajili watoto wasiojiweza na mayatima zone ya kikwajuni na maeneo ya karibu ila hatujaweza kuwapatia wafadhili wa uhakika ambapo ni wachache tu hua wanajitolea.
  3. Tumeweza kisaidia Madrasat Annour Islamia iliopo Mikunguni nyuma ya hospital ya  Utapoa kwa kuitafutia na kuiombea ipate ukarabati wa kujengwa na Alhamdulillah tunashukuru na ujenzi umetulia unaendelea.
  4. tumeweza kushiriki katika mashindano ya Qur-an kanda ya mjini pamoja na katika jumuiya ya kuinua vipaji vya kuhifadhi Qur-an kikwajuni.
  5. Tumeweza kufanikiwa suala la maghafali kila mwaka pamoja na futari nk.
WABILLAHI TAWFIQ



No comments:

Post a Comment