Umri Gani Huhesabika Kuwa Ni Mtoto Yatima?
Ifahamike kuwa yatima
katika Uislamu ni yule aliyefiliwa na baba, kwani aliyefiliwa na mama
haitwi yatima kabisa. Aliyefiliwa na wazazi wote wawili ni yatima zaidi
kuliko aliyefiliwa na baba peke yake.
Ama
umri wa mwanadamu kuitwa yatima ni kabla ya kubaleghe. Akisha baleghe
basi anakuwa si yatima tena. Umri wa kubaleghe inategemea mazingira,
jinsia, nchi na kabila pia. Ama kwa wasichana wanaweza kubaleghe kuanzia
umri wa miaka tisa na mvulana baada ya umri huo, sana sana kuanzia 15.
Na Allaah Anajua zaidi
NI KWANINI MADRASAT MAJALIS SANIA IMEAMUA KUWAKUSANYA WATOTO YATIMA
Kwanza tufahamu kuwa:-
Suala
la malezi ni jambo la wajibu katika Uislam, kwani mtu akosapo malezi ya
sawa bila ya shaka atakengeuka na atapotea, na kwa maana hiyo ndiyo
Uislam ukawapa wafuatao uwajibu wa kumhifadhi na kumlinda mtoto ili
asiangamie:
1.
Mama ana haki zaidi ya kuyasimamia malezi ya mtoto wake baada ya
kuachwa kwa talaka, au kifo, au kwa kuolewa na mume mwingine, na
atanyimwa haki hiyo pale tu patakapojitokeza vizuizi vitakavyolazimu
kufanya hivyo;
2.
Bibi upande wa mama, bibi upande wa baba, kisha madada, kisha mama
wadogo, kisha wapwa, kisha mabint wa kaka, kisha mashangazi, na kufuatia
ndugu wengine kama ilivyo kwenye utaratibu wa mirathi.
Ama
jukumu la kuharibika kwa mtoto, litamhusu kwanza yule aliyekuwa ndiyo
sababu ya mtoto kuharibika, pili litamhusu kila aliyeuona uharibifu huo
unatokea na akaunyamazia. Tutambue kuwa kila mtu mwenye jukumu lazima
atimize mas-uliya yake na kila mmoja wetu ataulizwa kuhusu jukumu hilo kama alivyotufundisha Mtume wetu (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((كلكم راع وكلكم مسئول عن رعيته الإمام راع ومسئول عن رعيته والرجل راع في أهله وهو مسئول عن رعيته والمرأة راعية في بيت زوجها ومسئولة عن رعيتها))
((Kila mmoja kati yenu ni mchungaji, na kila mmoja kati yenu atapaswa kuulizwa ya juu ya kile anachokichunga. Imaam ni mchungaji na ataulizwa kwa anaowachunga. Mume
ni mchungaji wa familia yake, naye atapaswa kuulizwa juu ya
anaowachunga. Na mke ni mchungaji wa nyumba ya mumewe, naye pia atapaswa
kuulizwa juu ya anachokichunga. (Al-Bukhaariy, Muslim)
Tukija
katika Suala la kulea yatima tutambue kuwa hili ni jukumu zaidi kwani
kulea yatima kuna fadhila nyingi na ujira wake ni mkubwa mno. Na
kutomlea vizuri pia kuna hatari yake.
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ametaja fadhila za Yatima mara nyingi sana katika Qur-aan, tutazitaja hapa chache:
((وَيَسْأَلُونَكَ
عَنِ الْيَتَامَى قُلْ إِصْلاَحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ وَإِنْ تُخَالِطُوهُمْ
فَإِخْوَانُكُمْ وَاللّهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ وَلَوْ
شَاء اللّهُ لأعْنَتَكُمْ إِنَّ اللّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ))
((Na
wanakuuliza juu ya mayatima. Sema: Kuwatengenezea ndio kheri. Na
mkichanganyika nao basi ni ndugu zenu; na Allaah Anamjua mharibifu na
mtengenezaji. Na Allaah Angelipenda Angelikutieni katika udhia. Hakika
Allaah ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima)) [Al-Baqarah: 2:220]
((يَسْأَلُونَكَ
مَاذَا يُنفِقُونَ قُلْ مَا أَنفَقْتُم مِّنْ خَيْرٍ فَلِلْوَالِدَيْنِ
وَالأَقْرَبِينَ وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا
تَفْعَلُواْ مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللّهَ بِهِ عَلِيمٌ))
((Wanakuuliza
watoe nini? Sema: Kheri mnayoitoa ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na
mayatima na masikini na wasafiri. Na kheri yoyote mnayoifanya Allaah
Anaijua)) [Al-Baqarah 2:215]
Na khaswa kwa vile ni jamaa yake wa damu anayemlea Amesisitiza Allah:
((فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ)) ((وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ)) ((فَكُّ رَقَبَةٍ)) ((أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَة)) (( يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ))
11. Hakuweza kuvikwea vikwazo vya milimani (njia nzito ya kukufikisha peponi)?
12. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani (njia ya kukufikisha peponi)?
13. (Kuvikwea vikwazo vya mlima huo ni) Kumkomboa mtumwa
14. Au kumlisha siku ya njaa
15. Yatima aliye jamaa
[Al-Balad: 11-14]
Vile vile kasema Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
((أنا وكافل اليتيم في الجنة هكذا)) وأشار بالسبابة والوسطى وفرج بينهما ( رواه البخاري)
((Mimi na mwenye kumlea Yatima kama hivi)) Akaashiria kidole cha shahada na cha katikatikati pamoja na akaviachanisha baina yake [Al-Bukhaariy]
Vile vile kasema
من وضع يده على رأس يتيم رحمة ، كتب الله له بكل شعرة مدت على يده حسنة. رواه الإمام أحمد
((Mwenye kuweka mkono wake kwenye kichwa cha Yatima kwa upole, Allah Humuandikia jema kwa kila unywele aliougusa kwa mkono wake)) [Imaam Ahmad].
Na katika kuwafanyia maovu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ametuonya:
((فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ))
((Basi yatima usimwonee)) [Adh-Dhwuhaa: 9]
((كلاَّ بَل لَّا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ))
((Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima)) [Al-Fajr: 17]
Shangazi wa huyo Yatima anapaswa kupewa nasiha amche Allah na atimize jukumu lake.
Na Allaah Anajua zaidi
Hivyo Madrasat Majalis Sania kitendo cha kuwakusanya watoto yatima na wasiojiweza hali zao ni kuwasaidia katika kuwatafutia wadhamini,misaada mbalimbali kwa sababu Imani yetu ni kuwaona watoto yatima hawapo katika hali ya unyonge zaidi hasa wale ambao hawana uwezo katika familia zao.Tunatoa wito kwa mtu yoyote ambae atakua na Uwezo wa kuwasidia watoto mayatima na wasio jiweza Inshallah Awasiliane nasi kupitia Madrasat Majalis saniua kwa marehemu maalim Bi Mkubwa Stadi Michenzani Mjini ZANZIBAR kwa nambari zifuatazo 0776721401 / 0715721401 Facebook - https://www.facebook.com/madrasatmajalis.sania
Bado tunaendelea kuwakusanya na kuwasajili watoto yatima ambapo tupo katika harakati za kujisajili katika Ofice ya mufti wa zanzibar ili tuzidi kufanikiwa malengo yetu
Matumaini yetu na malengo yetu yatatimia.
Namuomba Allah atusaidie.
UMOJA WA MAYATIMA ZONE YA KIKWAJUNI
14/02/2016 DUA YA MAYATIMA
KassimAli Abdallah,Muhammed Ali Abdallah na Omar Bakar Hamad ni watoto yatima
Ni watoto kutoka maeneo tofauti katika zone yakikwajuni wakipata sadaka baada ya dua
Ni maeneo ya kiswandui baada ya dua iliosomwa na watoto yatima ndani ya nyumba ya familia moja ambayo tulitakiwa kuwaombea wazee wao na watoto wao wafanikiwe katika yao,namuomba Allah aikubali dua...amin.
ORODHA YA MAYATIMA KATIKA MAENEO TOFAUTI YA ZONE YA KIKWAJUNI KUPITIA MADRASANI MWAO NA MITAANI
kiongozi wa Umoja wa watoto mayatima zone ya kikwajuni ni Ustadh Anasi khatibu Zubeir Muya
ambae ni mwalimu mkuu na msimamizi wa chuo cha marehemu maalimu Bi mkubwa stadi Al-madrasat Majalis Sania ambayo ipo Michenzani nyuma ya Blok no 5 ngazi ya 4.
ambae ni mwalimu mkuu na msimamizi wa chuo cha marehemu maalimu Bi mkubwa stadi Al-madrasat Majalis Sania ambayo ipo Michenzani nyuma ya Blok no 5 ngazi ya 4.
Lengo la kuwakusanya watoto mayatima ni kuwa wapate kusaidiwa ambapo wapo watu ambao huwa wanajitolea kuwasaidia lakini ni kwa kipindi ambapo mara nyingi hutokea misaada yao na huwa tunawakosa wapi pa kuwapatia,hivyo kutokana na hayo tumeona ipo haja ya kuwakusanya watoto mayatima kupitia madrasa zao na wengineo kupitia mitaani na nyumbani kwao.
MADRASA AMBAZO TUMEWAKUSANYA WATOTO YATIMA
- MADRASAT MAJALIS SANIA (BI MKUBWA STADI)
- MADRASAT MUUMIN (DAKSHI)
- MADRASAT JAILAN (BI DODO)
- MADRASAT ULAA (KIKWAJUNI KWA MSELEM)
- MADRASAT FATMA (KISWANDUI)
- MADRASAT SHADHLIA (MABATI)
- MADRASAT NURA NIA ISLAMIA (KWA BINIA)




No comments:
Post a Comment