Siku ya leo tumeweza kufika makaburi Mwanakwerekwe kwa ajili ya kuwaombea Dua walimu wetu Bi Mkubwa Stadi ambae amefariki siku kama ya leo 11-01-2010 na tukamzika 12-01-2010 na mwanawe Bi Mariam Hajji ambae alifariki 12-12-2013 na kumzika siku hio hio.
Mwalimu Bi Mkubwa Stadi alizaliwa mnamo mwaka 1926 na akaanzisha Al-madrasat Majalis Sania mwaka 1940 na na akazaliwa mwanawe Bi mariam Hajj mwaka 1944 Madrasa rasmin ilianza mwaka 1945 kisima majongoo kutokea kikwajuni kwa mujibu wa historia nilivyoipata, Mwalimu Bi mkubwa Stadi Alianza na wanafunzi wachache miongoni mwao ni Bi Sania Mahmoud ambae jina la Madrasa limetokana na Jina lake yeye Sania na ikapewa jina Rasmin kua Madrasat Majalis Sania Al-qadira jina hili nilipata kusimuliwa kua alilitoa Marehemu Sheikh Yahya Hussein ambae alimuoa mtoto wa Bi Siku ya leo tumeweza kufika makaburi Mwanakwerekwe kwa ajili ya kuwaombea Dua walimu wetu Bi Mkubwa Stadi ambae amefariki siku kama ya leo 11-01-2010 na tukamzika 12-01-2010 na mwanawe Bi Mariam Hajji ambae alifariki 12-12-2013 na kumzika siku hio hio.
Mwalimu Bi Mkubwa Stadi alizaliwa mnamo mwaka 1926 na akaanzisha Al-madrasat Majalis Sania mwaka 1940 na na akazaliwa mwanawe Bi mariam Hajj mwaka 1944 Madrasa rasmin ilianza mwaka 1945 kisima majongoo kutokea kikwajuni kwa mujibu wa historia nilivyoipata, Mwalimu Bi mkubwa Stadi Alianza na wanafunzi wachache miongoni mwao ni Bi Sania Mahmoud ambae jina la Madrasa limetokana na Jina lake yeye Sania na ikapewa jina Rasmin kua Madrasat Majalis Sania Al-qadira jina hili nilipata kusimuliwa kua alilitoa Marehemu Sheikh Yahya Hussein ambae alimuoa mtoto wa Bi mkubwa Stadi Bi Mariam hajji Mussa.
Siku zimetembea madrasa ilinawiri kuwa na wanafunzi wengi walio maarufu kwenye Zanzibar hii na walio wakawaida ambapo mwalimu aliweza kupata kuengeza jengo la madrasa ili wanafunzi wasome.
Kufikia miaka ya 1988 jengo lilikamilika na watoto wakawa wanapata Taaluma na huku harakati zikienda vizuri kwa mwalimu Bi mkubwa stadi ambae Pia aliwahi kusomesha Skuli ya Kiswandui na Sunni Madrasa Mkunazini.
Ilipofika miaka ya 2007/8 madrasa ilianza kufifia wanafunzi ikafikia hali ya Madrasa kubaki na wanafunzi Wawili tu ambao ni mjukuu wake na jirani yake,na sababu yake ni kutokana na Kupata Maradhi na kuishiwa na nguvu na kukosa mwalimu wa kudumu ili kuisimamia madrasa ingawa walipita wanafunzi wengi na walikua wakisimamia ila kutokana na hali na maisha hawakuweza kudumu madrasa kama inavyotakiwa.
Ilipofika miaka ya 2010 Mwalimu alifariki Dunia na akabakia mwanawe Bi mariam Hajji na akaisimamia madrasa na ndipo Akajitolea kwa moyo wa imani ndugu Bi Malik khatib Zubeir (Ustadh Anasi khatib Zubeir) akaisimamia madrasa na tukashirikiana na vijana waliopita na tukawarejesha waliopotea tukaamua pamoja na Miongoni mwa Familia akiwemo Ndugu Ibrahim Fataki na wengineo waliomfuata nyuma yake, pamoja na Msimamizi mkuu Ant Sania Mahmoud Allah amuhifadhi na tukaanza na wanafunzi 6 sita na leo hii wamefikia idadi ya wanafunzi 92 ukizingatia wapo waliokhitimu na kukimbia na dharura tofauti za kimaisha.
Na ndani ya Kirundi hiko tukaanza na Ujenz,Ujenzi ambao uliendeshwa na Bin malik khatib Zubeir pamoja na wanafunzi wote kwa kuwatafuta wadhamin kupitia Maeneo tofauti na hadi tumeweza kufanikiwa ujenzi umetimia Alhamdulillah tumepata Jengo Jipya ingawa tulipitia mitihani mingi sana ila ndio changamoto nasi tupo tunaiimarisha na kuendeleza madrasa isirudi ilipotoka.
Tunawashukuru sana wale wote walioweza kutusaidia katika Ujenzi wa madrasa na hata wale waliotupa mawazo yao nini tufanye pia tunawapa shukrani na wanaoendelea kutusaidia kwenye harakati hizi za kuiendesha madrasa kwasababu madrasa inajitegemea na kutegemea misaada kupitia Familia ambao pia tunawapa shukran kwa nguvu zao.
Mwisho tunamuomba Allah awashushie rehema walimu wetu na sisi tuliopo Allah atupe Subra hikma na Uvumilivu ili tuweze kudumu.
Ameen
Shukran
Ustadh Anasi khatib Zubeir
Katibu/Mwalimu Mkuu
No comments:
Post a Comment