Thursday, 20 August 2015

Mukhtasar wa harakati za ujenzi wa madrasa

Tunakumbuka ni wapi tulipotokea ambapo tulijawa na hofu na mawazo akilini na kujiuliza hivi ni lini tutafanikiwa ?, Tulipita nyingi ngazi kuweza kusimamia ujenzi wa madrasa yetu tukajitangaza kwa kuchuna nyuso zetu kwa kila muumini ili aweze kutusaidia, tunashukuru tuliweza kufanikiwa kwa baadhi ya watu waliojitokeza na kujitolea kutusaidia na walijitokeza watu wakatuahidi hadi leo ahadi zao hawakuzitimiza , na wengine walituchokoza kwa masihara mengi kutufanyia hadi kutishwa na kugombezwa na baadhi ya watu kuwa tusitangaze kuomba misaada kupitia mitandao na kuniambia futa jina la madrasa na nyingi shituma ambazo zilikua zinatuvunja moyo, lakini sikuchoka kuomba msaada hadi leo madrasa tumepiga hatua ambayo katika akili yangu zikuweza kufikiria kama tutafanikiwa ila nilikua namuomba mungu sana nashukuru tumefanikiwa ALLAH AWALIPE MAZUR I HAPA DUNIANI NA KESHO AKHERA wale wote waliotusaidia hata kwa mawazo kwani wapo wengine waliweza kunipa nasaha na kunielekeza njia gani nipite, lakini waliodhaifu waliweka ahadi na kutusimbulia na kuzani sisi ni wizi na mengi matatizo siyaishi yote kuyaeleza isipokua tu nasema tuanshukuru na kuwashukuru kwa wema wenu mliotufanyia ingawa ni bado madrasa haijamaliza kikamilifu lakini tumepiga hatua kubwa.
Nasaha zangu ni kwamba tujitahidi kutoa katika njia ya ALLAH (sw) na pia bado tunahitaji zulia limekua chakavu lina mavumbi mengi sana,Mnara wa kupachika Tanki ya maji hadi leo bado hakutokea mdhamini lakini vifaa vyote vya maji tumeshapata isipokua mashine tumeahidiwa tu na hadi leo haikupatikana Inshaallah Allah Atatuwezesha .
Pamoja na yote hayo Ipo madrasa nyengine niliwahi kuielezea hapa nayo ina matatizo ya uchakavu wa banda lao la kusomea na mwalimu wao ameshafariki ,kiukweli wapo katika hali duni ya chini sana kiasi hadi imebidi waniombe mimi niwasaidie nilichojitolea mimi ni kuwatangazia kama nilivyoitangaza madrasat majalis sania, Madrasa hiyo inaitwa madrasat ANNOUR ipo maeneo ya hospital ya Utapoa nyuma mtaa wa kwa juma pweza Umaarufu kwa bikei (Bi kijakazi) namba zao za simu ni
0773227528 ustadh yussuf - ANOOUR – Mikunguni Utapoa
0776721401 Ust Anasi khatib Zubeir – Majalis sania michenzani nyuma ya blok na 5 ngazi ya 4 nyuma
0715721401
TUNAOMBA KAMA UPO UWEZEKANO WA KUTULETEA VIFAA TU WALLAHI ITAKUA NI JAMBO KUBWA MOJA LA FARAJA .
WABILLAHI TAWFIQ

No comments:

Post a Comment