Wednesday, 16 May 2018

RAMADHAN MUBARAK

Madrasat Majalis Sania tunawatakia waislamu wote Ramadhan Mubarak

Monday, 30 April 2018

NI NAMNA GANI TUNAWASOMESHA NA KUHITIMU

AL-MADRASAT MAJALIS SANIA
Jumanne 01,May-2018 - 14,Shaaban-1439

Ni Chuo Cha Marehemu Maalim Bi Mkubwa Stadi kiliopo Michenzani Mjini Unguja,Zanzibar
Tunasomesha Qur-an na masomo mengine ya Dini ya Msingi ambapo madrasa yetu ina upana wa mita nane (8) na mita 15 Urefu ambapo pembeni yake imeungana na nyumba ya mwalimu ambapo hapo awali kabla ya jengo jipya alikua ndipo anaposomeshea.

Tuna madarasa  Saba ambapo ni Darasa la NURSERY-A- ni wale wanawafunzi wa umri wa miaka minne-mitano wanaoanza msingi wa Qur-an


Kuna NURSERY -B: Darasa hili ni kwa wale wa miaka minne - mitano waliokua wameshaweza kutamka kwa matamshi na kuzifaham herufi kwa njia ya kutofautisha na kuweza kuzibagua kwa namna ya mparaganyiko.
NURSERY- C : hili ni Darasa la watoto walioweza kuchanganya maneno kwa uzuri na kuzijua herufi kwa maumbo tofauti na yalioweza kuunganishwa kwa maneno kuanzia mawili na kuendelea.


DARASA LA KWANZA :Ni darasa la watoto kuanzia miaka 7- 9 ambao wanaoanza kusoma Juzuu ya Amma na kila siku moja huwa wanasoma aya 10 upande wa Suratul Nnabai na upande wa Suratul -Fat-ha husoma kwa Irabu kila siku sura 2, na mara nyingi ndani ya miezi 6 au mwaka mmoja huwa wameshahitimu juzuu ya Amma na kuendelea mas-haf.
DARASA LA PILI: hili ni darasa kuanzia umri wa miaka 10 hadi pale atakapo maliza selebas(Mada za darasa la kwanza)- wapo ambao hutokea kuhitimu mas-haf ndani ya darasa la pili ambapo hua wanasoma kupitia Time-Table.
DARASA LA TATU:Hili ni Darasa kuanzia umri wa miaka 11 hadi kuendelea maelezo yake ni kama ya darasa la pili ambapo pia darasa hili huwa wanasoma kwa njia mbili -Alefika juzuu ya 3 ataanza kusoma Suratul -Yasin - Hadi kukutana  kati baina ya upande wa juzuu ya tatu na Yasin na ikitokea kumaliza sura zote hua anaenelea Fatir na upande wa pili ataanza Alif Laam Bakra nao hufuata Time- Table hutokea kuhitimu kwenye darasa la tatu.
DARASA LA NNE: Ni Darasa Ambalo mara nyingi huanzia umri wa miaka 15 - na kuendelea(Balegh) na mara nyingi hua wameshahitumu Mas-haf  - utaratibu wa kusoma Qur-an ni wa Juzuu moja kwa kila siku na kwa wale ambao bado hawakuhitimu kutokana nasababu tofauti (kama utoro,kusahau,ufaham n.k) mara nyingi husoma kwa page mbili kila siku,

Pamoja na yote ni mara nyingi husoma Vitabu - Tafsiri ya Quran,Bulughul-maramiy, Riyadhu-Swalihin

Tunapokea kuanzia miaka 4 alichanganya maneno hadi miaka 15 tu madrasa yetu bado changa na ndio tunajitahidi tufikie malengo tuliyoyakusudia.

Chuo ni hazina kubwa na zawadi kutoka kwa walimu wetu Bi Mkubwa Stadi na Mwanawe Bi Mariam Hajji -Allahummaghfirlaha warhamha wamaskanha.

Yaa Allah tuongoze na utusimamie katika kuisimamia madrasat Majalis Sania na umuhifadhi Bi Sania mahmoud maalim Umpe Umri Mrefu wenye kheri ili azidi kushuhudia matunda ya madrasa alioachiwa na walimu wake.

Namuomba Allah aisimamie Familia ya Marehemu Mwalimu.

Amen

MADRASAT MAJALIS SANIA
(BI MKUBWA STADI)
Michenzani -Unguja,Zanzibar Tanzania
Email :Majalissani@gmail.com
Blogger : http/:bimkubwastadi.blogspot.com
Call:+255776721401
        +255715721401

Thursday, 4 January 2018

YALIKUA MAKARIBISHANO

Siku ya Alhamis 04,January 2018 tupo katika viwanja vya Madrasat Muumin Islamia Daksh kwa ajili ya Makaribisho ya Wageni wao kutoka Dar-es-salam Al-Madrasat Muumin Muqadim